DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Friday, 17 September 2021

AJALI YAUA WANAFAMILIA SITA (6) NA KUJERUHI TISA (9)

 

Na Amon Mtega ,Mbinga

WATU sita wanaodhaniwa kuwa  ni wanafamilia wamefariki Dunia na wengine tisa kujeruhiwa  kwa ajali ya gari lililoacha njia na kupinduka katika maeneo ya mteremko wa Kijiji cha Kipololo na Lundumato Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo amelitaja tukio hilo kuwa limetokea Septemba 16 mwaka huu majira ya saa nane mchana huko katika mteremko mkali wenye urefu wa zaidi ya kilometa 1,wa Kijiji cha Kipololo ambapo gari hilo lenye namba za usajili T.503 DWF Toyota Coaster mali ya Joseph Ferdinand Eugeni wa Dar es salaam liliacha njia kisha kupinduka na kutumbukia kwenye bonde lenye urefu wa takribani mita 120 wakati likielekea Wilaya ya Nyasa kwenye mambo ya kifamilia.

Kamanda Konyo amewataja marehemu kuwa ni Mohamed Hussen Athuman (37) ambaye alikuwa dereva wa gari hilo mkazi wa Mbezi Dar es salaam,Penzia Chale (60) mkazi wa Ukonga Dar es salaam,Franko Chale(40) mkazi wa Songea mjini, Joyce Ndonde (45) mkazi wa Tabata Dar es salaam,Gerald Ndonde (60)mkazi wa Songea mwalimu shule ya msingi Ruhuwiko ,na Jonson Chale(11) mwanafunzi wa shule ya msingi ambayo haikufahamika jina ya huko Dar es salaam.

Kamanda Konyo pia amewataja majeruhi kuwa ni Nathan Ndonde (60) mkazi wa majumba sita Dar, Godfrey Chale (40) mkazi wa Banana Dar, Nelson Ndonde (40)mkazi wa Tabata Dar,Amina Mpangala (34) mkazi wa Dar,Janeth Ndonde (35) mwalimu wa shule ya msingi ambayo haikufahamika jina ya huko Dar,Janeth Ndonde (33)mkazi wa Dar ambaye ni mfanyabiashara, Catherine Ndonde (45)muuguzi mkazi wa Dar na Patrick Mpangala (32) mkazi wa Tabata Dar.
Kamanda amesema majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya misheni ya Litembo Wilaya ya Mbinga huku miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbinga ikisubiri uchunguzi wa daktari kisha taratibu zingine zitafuata.

Hata hivyo kamanda Konyo ametoa rai kwa madereva wageni na barabara za mkoa wa Ruvuma kuacha tabia ya kutumia mazoea wanapoendesha vyombo vya moto (Magari)kwa kuwa barabara za Mkoani humo asilimia kubwa zinakona nyingi na miteremko mikali.

No comments: