DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Wednesday, 20 October 2021

MUME AMBAKA MKEWE HADI KIFO

 Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika pori la Mfyome wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa ambapo mwili wa marehemu ulikutwa eneo hilo huku pembeni kukiwa na kamba ya asili ya kufungia kuni pamoja nguo zake zikiwemo nguo za ndani huku shingoni akiwa na alama za kucha.



Akizungumza na matukio daima, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mfyome Richard Alyoce, amesema kuwa alipata taarifa za tukio hilo majira ya saa tatu asubuhi akiwa nyumbani kwake ambapo aliongozana mara moja na mtoa taarifa mpaka eneo la tukio.

''saa tatu asubuhi nikiwa nyumbani kwangu alikuja kijana akaniambia kuna eneo fulani nilikuwa nafanya usafi wa shamba nimemuona mtu jinsia ya kike kama kalala chini, nikamuuliza unahisi atakuwa amekufa? akasema ndio nahisi ameshafariki, nikamuita mwenyekiti wa kitongoji husika maana ndio eneo lake, tukaambatana mpaka eneo la tukio na tukamkuta aliyelala pale ni mwananchi aitwaye Salome Kisayo(43) huku pembeni kukiwa na kamba pamoja na nguo zake za ndani huku maeneo ya shingo kukiwa na kucha pamoja na alama za kukabwa'' alisema Richard

Mwenyekiti amesema kuwa walitoa taarifa polisi ambapo walipofika waliuchukua mwili mpaka hospitali ya mkoa, kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya hapo walikabidhiwa kwa ajili ya kwenda kuzika. Pia ameeleza kuwa mume wa marehemu aitwaye Belatus Kindole(60)  alitoweka walipokuwa mochwari ambapo mpaka sasa hajulikani alipo na simu zake hazipatikani.

''huyu mume kwanza kabla ya mimi kupata hizi taarifa alikuja kwangu juzi jumapili akaniambia anamtafuta mkewe salome, na alikuwa na barua ya kitongoji na mimi nikamuandikia barua nyingine ili aweze kwenda vijiji vingine na polisi kutoa taarifa, lakini mpaka inafika hiyo saa tatu asubuhi siku niliyopata taarifa kuja kushuhudia hili tukio nilimpigia simu baada ya kuona ni mke wake yule aliyekuwa anamtafuta, lakini ilimchukua kama lisaa hivi kufika hapa,  tukawa tupo wote mpaka tunaenda mochwari pamoja lakini kufika kule alikaa kidogo na akaondoka , tulipojaribu kumpigia simu zake zilikuwa hazipatikani mpaka muda huu tunaozika hayupo na hatujui yupo wapi'' alisema Mwenyekiti

Hata hivyo Richard amesema kuwa chanzo cha ugomvi wa marehemu na mumewe ni wivu wa kimapenzi ambapo mume hakutaka mkewe aende hata kwa jirani kusalimia kwani wangemfundisha tabia mbaya na hivyo aliona kufanya hivyo labda kutamfanya akae kwa amani na pia walikuwa wakipelekana mpaka polisi.

Na kwa upande wake Diwani wa kata ya Kihwele Felix Waya amesema kuwa hilo ni tukio la kwanza kutokea katika eneo hilo na limewashangaza sana na amewataka wananchi kutoa taarifa kwa uongozi kama kuna jambo lolote linawakwaza hata kama ndani ya ndoa na sio kujichukulia sheria mkononi. 

Nao ndugu wa marehemu wamewashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa ushirikiano walioutoa kwenye msiba huo mpaka kumpumzisha mpendwa wao katika safari yake ya mwisho na kuwaomba waendeleze  ushirikiano huo.


No comments: